Theolojia Katika Picha
3 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
14. E lewa kwamba sababu za kuandikwa, mila, na masuala ya maisha, ni mambo muhimu katika mchakato wa kutafsiri Maandiko. Kanuni lazima zieleweke, ziwe na mantiki na zenye utetezi; na ziendane na namna wakristo wametafsiri Maandiko katika kipindi chote cha historia; na lazima zisaidie kueleweka kutokana na namna ya maisha ya binadamu.
15. K wa umakini mkubwa ondoka kutoka kwa kile ambacho Maandiko “yalimaanisha” Kwenye hadhira ile ya asili mpaka kile “yanachomaanisha” Kwa msomaji wa sasa.
Kutumia Kanuni za Jumla kwa Sasa
16. T endea kazi kweli za jumla kwenye hali fulani mahususi ambazo watu wanakutana nazo leo. • Kumbuka kwamba Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wa kwanza katika kuitendea kazi kweli. Muulize yeye kwa ajili ya uongozi wake kuhusu maana kwa ajili ya matumizi ya siku za leo na kwa maombi tafakari kuhusu maana ya andiko. • Tafuta uongozi wa Roho Mtakatifu kwa kuangalia namna alivyowaongoza Wakristo wengine(kutoka ndani na nje ya dhehebu lako) kutafsiri maana na matumizi ya Maandiko kwa leo.
17. W eka kanuni na utendaji wake katika lugha ambayo inaleta maana kwa wasomaji wa sasa.
18. W eka mtazamo wako kwenye “malengo muhimu ya mwisho”. Lengo la kujifunza Biblia ni kumfanya msomaji akue katika maisha na upendo kwa Yesu Kristo, kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Sio maarifa peke yake bali kubadilishwa maisha ndio lengo haswa la kutafsiri Biblia.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software