Theolojia Katika Picha
3 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
B. Mtambue mwandishi wa kitabu, tarehe kisiwa ya kuandikwa kwa kitabu, kwanini kiliandikwa, na kiliandikwa kwa nani. Zana za msingi: Kamusi ya Biblia, Biblia ya muongozo, au kitabu cha mafafanuzi ya Biblia
C. Soma muktadha uliopo katika kifungu hicho cha Maandiko
Zana za msingi: A Standard Translation of the Biblia (ambayo haijafupishwa). • Tazama kuona wapi ambapo matukio “yanabadilika” katika kifungu chako cha Maandiko na hakikisha unatazama kifungu chote wakati wa mchakato wa utafsiri. • Soma vitu vyote vinavyokizunguka kifungu hicho cha Maandiko. Huwa ni kanuni ya msingi kusoma angalau sura moja kabla na sura nyingine baada ya sura ile iliyokusudiwa. • Kadri unavyochagua kifungu kifupi cha Maandiko ndipo hatari ya kupuuzia muktadha inaongezeka. Mithali ya zamani huwa iko sahihi inasema “andiko bila muktadha ni kisingizio”
D. Chunguza kifungu cha Maandiko kwa umakini. • Tambua nani anaongea na nani anaongeleshwa • Zingatia mawazo makuu na taarifa muhimu. - Tengeneza muhtasari wa kifungu hicho cha Maandiko - Tambua mawazo makuu. - Tafuta maneno na mifano iliyojirudia. - Tafuta uhusianao wa “kichocheo-na-matokeo” - Tafuta ulinganifu, utofauti na muunganiko
E. Soma Maandiko hayo katika tafsiri nyingine ya Maandiko.
Zana ya msingi: Tafsiri au matumizi ya maneno tofauti ya Maandiko kwa namna nyingine ambako kunatumia filosofia tofauti ya tafsiri na lile toleo la Maandiko ambalo unalitumia mara nyingi.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software