Theolojia Katika Picha
/ 3 5
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
• Andika swali lolote ambalo tafsiri hii mpya imeliibua akilini mwako na uwe makini katika kupata majibu yake unapoendelea kujifunza zaidi.
F. Soma andiko la namna moja na hilo kutoka katika sehemu nyingine za Maandiko. Zana ya msingi: Konkodansi na/au Biblia ambayo inahusisha marejeo. • Zingatia taarifa gani zimeongezwa kwenye kifungu unachosoma kutoka katika sehemu nyingine za Maandiko. • Kwanini mwandishi alichagua kuondoa baadhi ya taarifa na kuzisisitiza nyingine? Na hii ina faida gani kwa kuelewa dhumuni la mwandishi? Zana za Msingi: leksimu za Kiebrania na Kiyunani na Kamusi zenye mafafanuzi zinasaidia kuongeza kina cha uelewa wetu wa maana za neno na matumizi yake. Mafafanuzi ya kiexejetiki yanasaidia kuelezea muundo wa kisarufi na namna unavyoathiri maana ya andiko. • Zingatia maneno ambayo yametumika katika njia ya kipekee na mwandishi na aina ya namna anavyoitumia sarufi kama vile vitenzi au maneno yanayoonyesha ulazima wa jambo, vitenzi vinavyoonyesha tukio linaloendelea n.k H. Tambua tanzu (aina ya fasihi) na zingatia kanuni maalum zinazotumika kwa hiyo. Zana za msingi: Kamusi ya Biblia na kitabu cha Mafafanuzi ya Biblia • Kila aina ya fasihi lazima ichukuliwe kwa uzito kwa vile ilivyo. Hatutakiwi kutafsiri ushairi kwa namna moja na tunavyo tafsiri unabii, au masimulizi kwa namna moja na kauli za amri. I. Tafuta muundo wa kifasihi ambao unaweza kusaidia namna andiko linaeleweka. Zana ya msingi: Mafafanuzi ya kiexejetiki • Muundo wa kifasihi unahusisha tamathali za semi, sitiari, mifano, alama, muundo wa kishairi, muundo wa tungo mfuatano n.k G. Jifunze maneno na muundo wa kisarufi
Made with FlippingBook Digital Publishing Software