Theolojia Katika Picha

3 6 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)

J. Tambua matukio ya kihistoria na masuala ya kitamaduni ambayo yangeweza kuathiri watu au kuathiri mawazo kwa namna yalivyoelezewa katika kifungu cha Maandiko. Zana za msingi: Kamusi ya Biblia na kitabu cha mafafanuzi ya Biblia • Mara zote jiulize, “nini kilikuwa kinatokea katika historia na jamii ambacho kingeathiri namna hadhira walisikia ujumbe katika andiko hili?” K. Andika kwa ufupi kile ambacho unaamini mwandishi alikuwa anajaribu kusema na kwanini kilikuwa ni muhimu kwa hadhira ile ya asili. • Lengo lako katika hatua hii ni kuandika kweli za msingi za kifungu cha maaandiko kwa namna ambayo mwandishi na wasikilizaji wa asili wangeweza kukubaliana nazo kama wangezisikia.

Shabaha ya hatua hii ni kutambua ujumbe mkuu, kauli za amri, na kanuni katika sehemu ya Maandiko ambayo inafundisha kusudi la Mungu kwa watu wote.

Hatua ya Pili: Kutafuta Kanuni za Jumla

A. Orodhesha kwa muundo wa sentensi zile unazoamini kuwa ndio kanuni za jumla katika kifungu cha Maandiko na zinafaa kutumika na watu wote, kwa wakati wote na tamaduni zote.

B. Lingamisha kauli hizi na sehemu nyingine za Maandiko kwa ajili ya uwazi na usahihi. Zana za msingi: Konkodansi, Biblia yenye mfumo wa mada Jiulize: • Kanuni nilizoziainisha zinakubaliwa na vifungu vingine vya Maandiko katika Biblia? • Ni zipi kati ya kanuni hizi zinaweza kuwa ngumu au haiwezekani kuzielezea pale zinapolinganishwa na vifungu vingine katika Maandiko?

Made with FlippingBook Digital Publishing Software