Theolojia Katika Picha
/ 3 7
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
• Je lazima kanuni yoyote kati ya hizi itengwe baada ya kuzama vifungu vingine vya Maandiko? • Ni taarifa gani mpya kuhusu Mungu na mapenzi yake kanuni hii inaongeza kwenye uelewa wangu wa jumla wa Maandiko na fundisho la imani? C. Rekebisha kauli zako za kanuni za Mungu kulingana na ugunduzi ulioufanya hapo juu. • Andika upya kanuni yako ya msingi kuakisi maarifa yaliyopatikana kutoka sehemu nyingine za Maandiko D. Soma mafafanuzi ya Biblia ili kugundua baadhi ya kanuni za msingi na mafundisho ambayo wengine katika Kanisa wameyapata kutoka katika kifungu hiki cha Maandiko. • Linganisha na tofautisha taarifa kutoka kwenye mafafanuzi na kujifunza kwako binafsi. Uwe tayari kuziacha, kubadilisha, au kutetea mtazamo wako kila unapopata taarifa mpya.
E. Kwa mara nyingine tena, rekebisha au boresha kauli zako za kanuni za Mungu kulingana na ugunduzi ulioufanya hapo juu.
Shabaha kubwa katika hatua hii ni kuhama kutoka kile Maandiko “yalimaanisha” Mpaka kile Maandiko “yana maanisha” Je utii kwa sheria na kusudi la Mungu unaonekanaje kwa nyakati hizi katika utamaduni wetu, na familia na marafiki zetu, pamoja na matatizo na fursa tunazokumbana nazo katika maisha yetu?
Hatua ya tatu: Kuzitendea kazi Kanuni za Jumla Leo
A. Muombe Mungu aongee nawe na akufunulie maana ya kifungu hiki cha Maandiko kwa ajili ya maisha yako. • Tafakari juu ya kifungu hicho cha Maandiko na vitu ulivyojifunza kutoka kwenye somo lako huku ukimuomba Roho Mtakatifu kukuonyesha maeneo mahususi ya kutendea kazi ya hizo kweli zilizogunduliwa kwa ajili yako na wale wanaokuzunguka.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software