Theolojia Katika Picha

7 6 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Jinsi ya kuanza kusoma Biblia Mch. Don Allsman na Mch. Dkt. Don L. Davis

1. Soma kipekee kila fungu, maandiko na hata vitabu katika mtazamo wa muktadha wa hadithi yote ya Biblia. Inaingiaje katika mpango wa ukombozi wa Mungu wa kuokoa chote kilichopotea wakati wa anguko?

2. Chunguza hali. Jiweke katika mandhari ukizingatia mazingira, sura ya mahali, harufu. Fikiria ilikuwa inafanana namna gani?

3. Uwe mwangalifu kwa amri, maonyo, maelekezo na misukumo inayofanya uwe na namna yakuishi nakufikiri ili uutafute kwanza ufalme wa Mungu.

Jinsi ya kusoma Biblia yote

Mpango wa kusoma Biblia #1:- kutoka Mwanzo hadi Ufunuo 1. Anza kwa kusoma kitabu cha Yohana kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hii itakupa muhtasari wa maisha yaYesu na kukusaidia kupata mambo ya msingi unaposoma sehemu yote

2. Rudi Mwanzo ukurasa wa kwanza na na soma Biblia yote

3. Usikwamishwe na vipengele, lakini soma kupitia Biblia nzima, kufurahia utajiri na aina nyingi andika maswali uliyonayo juu ya maneno usiyoyaelewa au mambo yanayokuchanganya ili uweze kumwuliza mtu, au kuja kuyaangalia baadae. Mpango wa kusoma Biblia #2:- mwongozo na mpangilio wa kusoma (www.tumistore.org) Unaweza pia kusoma Biblia kutoka mwanzo hadi mwisho kila mwaka, kusoma vitabu mbalimbali kwa mpangilio ambao wasomi Wakristo wanaamini iliandikwa. Waumini wengi husoma maandiko pamoja kila mwaka “kwa mpangilio” (kupitia wakati), wakitafuta kupata utambuzi wa hadithi yote ya Mungu jinsi ilivyotokea katika mpangilio wa matukio katika historia .

Made with FlippingBook Digital Publishing Software