Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 0 9
U O N G O F U & W I T O
C. Kuishi kamamgeni nampitaji huturuhusu kutumia rasilimali za ulimwengu kwa utukufu wa Mungu bila kuzidiwa nazo.
1. Kama wasafiri, hatutafuti mahali pa kudumu hapa, kwa hiyo tunawekwa huru kwenda popote pale ambapo Bwana anatuita. Hatuna anwani ya kudumu katika ulimwengu huu.
2. Kama wasafiri, tunaweza kuhama popote anapotaka tunapomwitikia Roho wake.
3. Tunayo shauku kubwa sana ya kwenda kwenye makao yetu halisi, jambo ambalo huturuhusu kuwa wawazi na wenye utayari wa kiwango cha juu zaidi katika mazungumzo yetu na Yesu Kristo kwa wengine.
III. Wito wa Ufuasi Pia Unahusisha Wito wa Kuishi kama Watumishi wa Kujidhabihu kwa Utukufu wa Yesu Kristo.
ukurasa 201 6
4
A. Tumeitwa kuzaa matunda, ili kwamba Baba apate kutukuzwa.
1. Baba hutukuzwa kwa vile ambavyo sisi kama wanafunzi wa Kristo tunavyozaa matunda mengi (Yohana 15:8).
2. Matunda tunayozaa katika jina la Kristo kwa utukufu wa Baba yamekusudiwa kuwa matunda yanayokaa – yaani yanayodumu, na mengi – maishani mwetu, katika sifa zetu, na katika huduma zetu, Yoh 15:16.
B. Ili kumletea Mungu utukufu, ni lazima tukumbatie maisha ya utumishi wa kujidhabihu, tukionyesha utayari wa kufa kwetu ili tuwe huru kuishi kwa ajili ya Kristo na Ufalme wake pekee.
1. Ni lazima tuwe tayari kudhabihu mengine yote kwa ajili ya jina lake na utukufu wake, Flp. 3:7-8.
Made with FlippingBook flipbook maker