Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 1 1
U O N G O F U & W I T O
Hitimisho
» Neno linatuita kwenye ufuasi , kushiriki katika hadithi ya ufalme mkuu wa Mungu katika maisha ya kujitoa ya ufuasi. » Tumeitwa kumpenda Yesu kwa upendo mkuu , zaidi ya ndoa na familia, kwa njia ambayo utukufu wake na mapenzi yake yanachukua nafasi ya kwanza katika maisha yetu. » Tumeitwa kuishi kama wageni na wasafiri katika ulimwengu huu , tukiishi maisha ya uhuru ili tuweze kupatikana kwake vyovyote na kokote anakotuongoza. » Tumeitwa kuwa watumishi wa kujidhabihu kwa utukufu wake , tukifa kwa nafsi zetu ili tuishi kwa utukufu wake. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibumaswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Jibu maswali yaliyo hapa chini, hakikisha unaelewa mawazo muhimu kuhusu jinsi Neno linavyotuita kuishi maisha ya ufuasi, chini ya ubwana wa Yesu Kristo. Tafadhali jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Kuna uhusiano gani kati ya Neno la Mungu ambalo linatuita kutubu na kumwamini Yesu Kristo, na Neno lile lile linalotuita kuishi kama wanafunzi wa Yesu? Elezea jibu lako. 2. Ni nini kinachohusika katika “kumpenda Yesu kuliko vitu vingine vyote,” kutia ndani ndoa na familia? Je, tunapaswa kuutafsirije uaminifu wa mtu kwa Yesu ukilinganishwa na utii mwingine wowote? Elezea. 3. Kuna uhusiano gani kati ya kuishi kwa uaminifu kama mfuasi wa Yesu Kristo mwenye msimamo thabiti na kupitia mateso? Je, kuna njia yoyote tunaweza kuepuka mateso hayo, na bado tukabaki kuwa wafuasi wa Yesu? 4. Inamaanisha nini kusema kwamba tunapaswa “kukubali utambulisho wetu mpya katika Kristo kama wageni na wasafiri katika ulimwengu huu”? Maandiko yanasema nini kuhusu wale wanaodai kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu na bado wanaupenda ulimwengu na mifumo yake ya uovu? 5. Kama wawakilishi wa Ufalme wa Mungu unaokuja, Wakristo wanapaswa kutafuta kwa kadiri gani kupata utajiri, umaarufu, na mamlaka ya ulimwengu? Elezea kwa umakini jibu lako.
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 201 7
4
Made with FlippingBook flipbook maker