Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
5 2 /
U O N G O F U & W I T O
2. 1 Wafalme 8:39 – basi… ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote).
3. Ayubu 34:11 – Kwani atamlipa binadamu kwa kazi yake, Naye atamfanya kila mtu kuona sawasawa na njia zake.
4. Zaburi 62:12 – Maana ndiwe umlipaye kila mtu Sawasawa na haki yake.
5. Mithali 24:12 – Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
2
6. Isaya 40:10 – Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.
7. Yeremia 17:10 – Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
8. Yeremia 32:19 – Mkuu wa mashauri, mweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake.
9. Ezekieli 18:30 – Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU.
10. Wakolosai 3:23-25 - Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.
Made with FlippingBook flipbook maker