Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
5 4 /
U O N G O F U & W I T O
Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa katika video kuhusu uwezo wa Neno la Mungu wa kuthibitisha kwa habari ya dhambi, haki, na hukumu. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Tunapaswa kuelewaje uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Maandiko Matakatifu? Je, ni sahihi kusema kwamba huduma ya Roho hufanya kazi, miongoni mwa njia nyinginezo, kupitia Neno la Mungu, ambalo limevuviwa kwa pumzi ya Mungu mwenyewe? 2. Ni kwa njia zipi Maandiko yanauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi? Je, tunapaswa kuelewaje dhambi kama dhana katika Agano la Kale? Vipi kuhusu dhana hii hii katika Agano Jipya? 3. Eleza mambo manne kuhusu haki yanayozungumziwa katika Maandiko. Kwa nini ni muhimu kuelewa vipengele hivi tofauti tunapozungumza juu ya uwezo wa Neno la Mungu wa kuuthibitishia ulimwengu kuhusu haki? 4. Ni kwa njia gani haki ya Mungu inafanyika haki yetu, tuliyohesabiwa (tuliopewa) na Mungu mwenyewe? 5. Neno la Mungu linaelezaje kusudi la Mungu la kuhukumu wanadamu? Mungu atawahukumu watu wote kila mahali kwa msingi gani, kulingana na Maandiko? 6. Orodhesha baadhi ya vikundi na vyombo ambavyo Mungu anakusudia kuleta hatimaye hukumuni. Je, tunajifunza nini kuhusu Mungu kupitia mafundisho ya Maandiko kwa habari ya nia yake ya kuhukumu ulimwengu wote? 7. Neno la Mungu huuthibitishiaje ulimwengu kwa habari ya hukumu? Kuna uhusiano gani kati ya hukumu za Mungu katika ulimwengu na Injili ya Yesu Kristo?
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 186 10
2
Made with FlippingBook flipbook maker