Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 5 5

U O N G O F U & W I T O

Neno Linalothibitisha Sehemu ya 2

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Katika sehemu hii tutagundua uwezo wa Neno la Mungu kuthibitisha kuhusu asili ya ukweli, na hivyo tutajifunza juu ya uwezo wake wa kubadilisha maisha na mitazamo yetu kupitia Roho Mtakatifu. Neno la Mungu limeweka wazi ufunuo wa Mungu kwa njia ya Kristo, Hadithi ya Ufalme kama msingi wa fundisho kuu la Mungu katika Maandiko yote, na ukamilifu wa Biblia ambayo ni matokeo ya utendaji wa Roho Mtakatifu kupitia manabii na Mitume waliovuviwa. Ushuhuda wao unayapa Maandiko mamlaka ya mwisho kwa habari ya imani na matendo (mwenendo), na kuyapa sifa ya kutegemewa kabisa katika mambo ya hukumu na kweli. Lengo letu la sehemu hii ya pili ya Neno Linalothibitisha ni kukuwezesha kuelewa na kueleza kwa wengine ukweli kwamba: • Neno la Mungu hututhibitishia kwa habari ya kweli. Neno la Mungu limevuviwa na Roho Mtakatifu na linahusishwa na Mungu wa kweli ambaye hawezi kusema uongo. Kwa hiyo, ni ushuhuda wa Mungu usioshindwa na rekodi ya ukweli usiobatilika. Inathibitisha kuhusu asili ya ukweli, yaani, yaliyo kweli kumhusu Mungu, kazi yake ulimwenguni, na hatima na kusudi la wanadamu. • Neno la Mungu pia huthibitisha kuhusu mada kuu ya Maandiko: ufunuo wa nafsi na kazi ya Yesu Kristo. • Neno la Mungu pia linathibitisha kuhusu usuli mkuu wa ufunuo wote wa Mungu: ufunuo wa mpango wake wa ufalme. • Neno la Mungu huthibitisha kupitia uadilifu wa wajumbe waliochaguliwa na Mungu, manabii na Mitume, ambao walipewa kazi ya kumwakilisha Mungu, kuzungumza juu yake na kuufafanua mpango wake.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

2

Made with FlippingBook flipbook maker