Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
5 6 /
U O N G O F U & W I T O
I. Neno la Mungu Linatuthibitishia kuhusu Ukweli kupitia Mada yake ya Msingi: Ufunuo wa Yesu Kristo na Kazi Yake.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
A. Mada kuu ya Maandiko ni Yesu Kristo. Ufahamu juu ya Yesu ndio ufunguo muhimu zaidi wa kihemenetiki wa kufasiri Biblia .
ukurasa 186 11
Yohana 17:17-19 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. 19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
1. Katika Barabara ya Emau, Yesu alijitangaza mwenyewe kwa wasafiri wawili kama ufunguo wa kufasiri Maandiko, Luka 24:25-27.
2. Baada ya kufufuka kwake, Yesu aliwafundisha Mitume wake jinsi alivyokuwa kitovu cha tafsiri ya Biblia kwa sababu ya mateso, kifo na ufufuo wake, Luka 24:44-48.
2
3. Yesu aliwakemea Mafarisayo kwa jinsi walivyotumia vibaya Maandiko walipokuwa wakiyasoma kwa bidii kubwa lakini wakashindwa kumwona Yeye kama mada na ujumbe mkuu wa Maandiko yenyewe, Yoh. 5:39-40.
4. Mwandishi wa Waebrania anarejelea nukuu kutoka kwa mpakwa mafuta wa Mungu ambaye anatambua nini kitabu cha Mungu kinasema juu yake, Ebr. 10:5-7.
5. Hatimaye, Yesu anathibitisha katika Mahubiri ya Mlimani kwamba hakuja kutangua Torati na Manabii bali kuitimiliza, Mt. 5:17.
B. Maandiko yanaomwonyesha Yesu Kristo kama kiini cha ujumbe na mada ya Biblia.
1. Yesu ndiye Mfafanuzi wa Mwisho wa Maandiko katika tafsiri yake ya Agano la Kale, ( taz. Mahubiri ya Mlimani, Mt. 5-7).
Made with FlippingBook flipbook maker