Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 5 7
U O N G O F U & W I T O
2. Yesu ndiye ufunguo wa vipengele vyote vya mfumo wa dhabihu katika Agano la Kale.
a. Yeye ndiye dhabihu ya Pasaka , 1 Kor. 5:7.
b. Yeye ndiye Kuhani Mkuu anayezungumzwa kwa habari ya Siku ya Upatanisho ya Agano la Kale, Ebr. 9:13-14; 10:11-14.
c. Anapita ukuhani wa Haruni , akiwa mfano wa ukuhani mkuu wa Melkizedeki, Ebr. 7:1-28.
2
d. Yeye ndiye utimilifu wa Hekalu (analinganisha mwili wake na Hekalu lenyewe), Yoh. 2:18-22.
3. Yesu anahusishwa na nafsi na kazi ya Mungu katika Agano la Kale.
a. Yeye ni Bwana juu ya kiti chake cha enzi, maono ya Yehova aliyopewa Isaya. (1) Isaya 6:1-13 (2) Taz. Yohana 12:37-41. b. Kama Neno aliyefanyika mwili, Yesu anawakilisha ufunuo wa mwisho na wenye mamlaka wa Mungu kwa wanadamu na kwa ulimwengu. (1) Yohana 1:18 (2) Waebrania 1:1-3 (3) Yohana 14:6.
Made with FlippingBook flipbook maker