Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

5 8 /

U O N G O F U & W I T O

II. Neno Linatuthibitishia kuhusu Ukweli kupitia Muhtasari wake wa Mpango wa Ufalme wa Mungu katika Agano na Ibrahimu na Utimilifu wake katika Yesu Kristo.

ukurasa 187  12

A. Yesu ndiye mada inayounganisha maagano yote mawili ya Maandiko.

1. Kulingana na Yohana Mtume, Yesu Kristo alikuja ulimwenguni ili azivunje kazi za yule mwovu (1 Yoh. 3:8).

2. Kwa sababu ya uasi wa Adamu na Hawa katika Anguko, wanadamu wamefanywa watumwa wa dhambi, wamesetwa chini ya laana, na hivyo kuishi katika utumwa wa hofu na uonevu wa kifo (kifo cha kimwili na kile cha kiroho, yaani kutengwa na Mungu).

2

3. Lakini, kwa sababu ya fadhili zenye upendo na rehema za Mungu, alimtuma Mwanawe kulipa adhabu ya dhambi zetu, na kuharibu dai la Ibilisi juu ya wanadamu na uumbaji wote, Tito 2:11-14.

B. Mpango wa Mungu wa kuwakomboa wanadamu ulifunuliwa katika agano na Ibrahimu.

1. Mungu alitoa ahadi ya kiagano kwa Ibrahimu, Mwa. 12:1-3.

a. Kumfanya kuwa taifa kubwa

b. Kumbariki na kulikuza jina lake

c. Kuwabariki watakaombariki na kuwalaani watakaomlaani

d. Katika Ibrahimu jamaa zote za dunia zitabarikiwa.

Made with FlippingBook flipbook maker