Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 6 1

U O N G O F U & W I T O

2. Sura ya 17 ya Injili ya Yohana 17 inatoa ufahamu mkubwa kuhusu jukumu la kipekee la Mitume kama wawasilishaji wa ufunuo wa Mungu. Kama wajumbe wake wateule, Yesu anawapa Mitume mamlaka na ushuhuda wa kipekee, anaposema kwamba:

a. Aliwafunulia jina la Baba.

b. Yote ambayo Baba alimpa Yesu yalijulikana kwao.

c. Yesu aliwawapa Mitume neno la kweli la Baba liletalo wokovu.

2

d. Ushuhuda wa Mitume kwa habari ya Kristo ungekuwa njia ambayo kwayo ulimwengu ungepata kuamini.

3. Kanisa limeipa jina la “utume” kanuni hii ya umuhimu wa Mitume katika maisha na imani ya Kanisa.

4. Neno la Mitume, kama wawakilishi wa Yesu mwenyewe, lina hadhi ya kimamlaka katika uelewa wa Kanisa kuhusu nafsi na kazi ya Yesu.

a. Paulo anaeleza kwamba nyumba ya Mungu “imejengwa juu ya msingi wa Mitume na manabii, Kristo Yesu mwenyewe akiwa jiwe la pembeni,” Efe. 2:20.

b. Tetea amana ya kitume: “mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu,” Yuda 1:3.

c. Kuna madhara ya kutisha kwa wale wanaofundisha mambo kinyume na mafundisho ya Mitume, Gal. 1:8-9.

Made with FlippingBook flipbook maker