Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
6 2 /
U O N G O F U & W I T O
d. Paulo anawakabidhi Wakorintho amana ya kitume ya Injili, yaani, kile alichopokea kutoka kwa Kristo na Mitume wake, jambo ambalo linaipa amana hiyo mamlaka ya mwisho na sifa kamili ya kuaminika, 1 Kor. 15:1-8.
5. Maandiko ya Agano Jipya ni neno la Mitume katika maandishi, na kwa hiyo yanabeba mamlaka ya Kristo kwa wale wanaoamini, 2 Pet. 3:15-16.
Hitimisho
» Neno la Mungu linatuthibitishia kwa habari ya kweli.
2
» Neno la Mungu lina uwezo wa kuthibitisha kuhusu asili ya ukweli, na hivyo kutuwezesha kujifunza uwezo wake wa kubadilisha maisha na mitazamo yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu. » Yesu wa Nazareti ndiye mada kuu ya ufunuo wa Mungu, na ujumbe wake wa hadithi ya ufalme unatumika kama msingi wa mafundisho katika Maandiko yote. » Neno la Mungu lina ukamilifu wa hali ya juu kutokana na namna linavyohusishwa na Yesu, manabii na Mitume waliovuviwa. Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kufanya mapitio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video. Yamekusudiwa kukusaidia upitie dhana muhimu zinazohusishwa na uwezo wa Neno la Mungu kuthibitisha kuhusu kweli ya Yesu Kristo, Ufalme wa Mungu, na ukamilifu wa ushuhuda wa manabii na mitume kwa habari ya imani. Tafadhali jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Maombi ya Yesu kama kuhani mkuu katika Yohana 17 yanatusaidiaje kuelewa asili ya Neno la Mungu kwa habari ya kutusaidia kuielewa kweli? 2. Je, tuna ushahidi gani wa kibiblia unaothibitisha kwamba Yesu Kristo mwenyewe ndiye mada kuu ya Biblia?
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 187 14
Made with FlippingBook flipbook maker