Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 6 3

U O N G O F U & W I T O

3. Ni kwa njia gani mahususi tunajua kwamba Yesu, kwa maana halisi, ni utimilifu wa mfumo wa Agano la Kale wa kumkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu? 4. Namna gani Yesu anahusishwa kwa ukaribu na ufunuo wa Baba katika Agano la Kale? Analo jukumu gani la pekee katika kutufunulia (kutujulisha) Baba?” 5. Je, hadithi ya uaminifu wa agano la Mungu kwa Ibrahimu inatusaidiaje kuelewa ukweli wa Maandiko kuhusu kazi ya Mungu ulimwenguni? 6. Ni kwa jinsi gani ufunuo wa Mungu kupitia wajumbe wa aina tatu (yaani, manabii, Yesu Kristo, na Mitume) unasaidia kututhibitishia kwamba Maandiko ni ya kweli, yaani, ni ushahidi wa kutegemewa na halali wa kile ambacho Mungu amefanya na atafanya duniani? Somo hili limejikita katika uwezo wa Neno la Mungu wa kuzalisha uthibitisho katika viwango mbalimbali, ambavyo vyote hutuongoza katika uhusiano na Mungu wa ndani zaidi, tajiri, na wenye ladha tofauti tofauti zaidi kwa njia ya Yesu Kristo. Neno la Mungu linatuthibitishia kuhusu dhambi, haki, hukumu na kweli. ³ Neno laMungu ni chombo chaRohoMtakatifu anachotumia kuuthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. ³ Maandiko yanafundisha kwamba dhambi inajumuisha chochote ambacho hakipatani na tabia kamilifu ya Mungu, sheria, na mapenzi yake. Dhambi na athari zake huwagusa wanadamu wote, ni za ulimwengu mzima katika upeo wake na zina asili ya uharibifu. ³ Sheria ya maadili ya Mungu, kama sehemu muhimu ya Neno la Mungu, hututhibitishia kwa habari ya dhambi zetu, ikifunua umbali uliopo kati ya matendo yetu na wajibu wa kimaadili wa matakwa matakatifu ya Mungu. ³ Neno la Mungu linathibitisha kuhusu haki. Linadhihirisha kupungua kwetu katika kuishika Sheria ya Mungu, na vile vile linaifunua haki ya Mungu kwa imani kupitia kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. ³ Neno la Mungu linathibitisha kuhusu hukumu, likieleza kwa usahihi na kwa nguvu kusudi la Mungu la kuhukumu wanadamu wote kulingana na matendo yao, kwamba ni walio hai au waliokufa. Katika utimilifu wa enzi,

2

MUUNGANIKO

Muhtasari wa Dhana Muhimu

ukurasa 188  15

Made with FlippingBook flipbook maker