Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
6 4 /
U O N G O F U & W I T O
Mungu pia atawahukumu Israeli na mataifa, Kanisa, Shetani na malaika zake, na waovu wote waliokufa. ³ Likiwa limehusianishwa kwa ukaribu na nafsi ya Mungu kupitia Yesu Kristo, Neno la Mungu huzalisha uthibitisho kuhusu asili ya kweli, yaani, yaliyo kweli kumhusu Mungu, kazi yake ulimwenguni, na hatima na kusudi la wanadamu. ³ Yesu Kristo mwenyewe ndiye mada kuu na ujumbe mkuu wa Maandiko, utimilifu wa mfumo wa dhabihu wa Agano la Kale, na ambaye pekee ameufunua utukufu wa utatu wa Mungu asiyeonekana. ³ Mpango wa ufalme wa Mungu umefunuliwa katika Maandiko kupitia ahadi ya agano la uaminifu la Mungu kwa Ibrahimu, na utimilifu wake katika Yesu Kristo. Neno la Mungu hututhibitishia kwa habari ya ukweli wa nia yake ya kuokoa watu kwa ajili yake, kutoka miongoni mwa familia zote za dunia, kwa njia ya Yesu Kristo. ³ Ukamilifu wa Neno la Mungu unaimarishwa kupitia uadilifu wa wajumbe waliochaguliwa na Mungu, manabii na Mitume, ambao walipewa kazi ya kumwakilisha Mungu na kuzungumza juu ya nafsi yake na mpango wake. Sasa ndio wakati wa wewe kujadiliana na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu Neno la Mungu na uwezo wake wa kuthibitisha kwa habari ya dhambi, haki, hukumu, na kweli. Kuhudumu katika miji ya Amerika kunadai ujuzi kwa kina wa Neno hili, ambalo hupenya na kufanya kazi ndani ya mioyo ya wale wanaolisikia ili kuwathibitishia juu ya ukamilifu na ukweli wake. Katika kufikiria juu ya nguvu ya uthibitisho ya Neno la Mungu, ni maswali gani hasa uliyo nayo kwa kuzingatia maarifa ulizojifunza hivi punde? Pengine baadhi ya maswali hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, ni lazima mwalimu au mhubiri aliamini Neno la Mungu ili liweze kuwathibitishia wengine kuhusu dhambi, haki, hukumu na kweli? Elezea jibu lako. * Je, Neno la Mungu huzalisha kiwango sawa cha uthibitisho ndani ya mwamini na asiyeamini? Kwa namna gani? Taja mifano. * Je, Roho Mtakatifu hutoa uthibitisho wa dhambi, haki, na hukumu mbali na Neno la Mungu? Ikiwa ndiyo au siyo, eleza kwa nini? * Je, mtindo wa uwasilishaji au namna Neno la Mungu linavyohubiriwa au kufundishwa huathiri uwezo wake za kuthibitisha? Kwa namna gani?
2
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
ukurasa 188 16
Made with FlippingBook flipbook maker