Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 7 5

U O N G O F U & W I T O

Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa Milele na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunakuita “Aba!” kwa kuwa wewe ni Baba yetu kwa imani katika Mwanao. Kupitia imani katika Injili ya Yesu Kristo, umetugeuza, umetupa maisha mapya, umetubadilisha kwa kutengeneza upya maisha yako ndani yetu. Tuseme nini, kwa namna ambavyo umetufanya kuwa watoto wako mwenyewe! Nia yetu moja ni kuwa kama wewe, Baba, tufanane na Ndugu yetu Mkubwa, Bwana Yesu, na kukutii kabisa, kukupendeza katika mambo yote, kuakisi sura yako katika kila jambo tunalofanya. Utujaze kwa Roho wako ili tudhihirishe ishara za kule kugeuzwa na wewe siku baada ya siku, hata tutakapokuwa zaidi na zaidi kama Mwanao. Kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu, Amina! Bwana Mungu Mpendwa, Mimi ni Kiumbe Wako—nimeumbwa na Wewe na kuwekwa hapa kwa mapenzi Yako. Nimepitia magumu mazito na kubeba majaribu makubwa. Nipe neema Yako ili nitambue hakika kuwa mimi ni wako na wewe ni Baba yangu. Nikungojee ili kupata msaada na usalama. Amina. ~ Martin Luther. Devotions and Prayers of Martin Luther . Trans. Andrew Kosten. Grand Rapids: Baker Book House, 1965. uk. 27.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

ukurasa 191  3

3

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 2, Neno Linalothibitisha .

Jaribio

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Yohana 16:7-11.

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukabidhi

MIFANO YA REJEA

Hilo ni Jambo la Kidini sana Kwangu

Katika kufahamiana na mmoja wa majirani zake, Hosea anagundua kwamba alikuwa akishiriki sana katika shughuli za Kikristo na kwenda kanisani. Kwa miaka mingi, familia hii jirani ilihudhuria kanisa ambalo lilisisitiza ishara za nje za imani

1

ukurasa 192  4

Made with FlippingBook flipbook maker