Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

7 6 /

U O N G O F U & W I T O

ya ndani. Kwa maneno mengine, waliweka mkazo zaidi kwa habari ya kufanya matendo mema ili kuonyesha kwamba wewe kweli ni mali ya Mungu. Kama familia yenye nidhamu na iliyopendezwa na masuala haya, kaya hii ya jirani ilihusika sana katika nyanja zote za maisha ya kanisa – kwaya na huduma za ibada, elimu ya Kikristo, na wajibu wa kutunza watoto wadogo kanisani, kwa kutaja machache. Baada ya muda, kanisa hili liliajiri mchungaji mpya ambaye alianza kufundisha kwamba kujihusisha na shughuli nyingi katika kanisa hakutoshi kwa mtu kuwa na uhusiano na Mungu. Inabidi mtu aokoke, yaani azaliwe mara ya pili. Mkazo huo mpya ulikuwa mgumu kwa familia hii jirani kukubali, kwa kuwa waliamini kwamba walipaswa kufuata dini kwa yale waliyoyatenda. Lugha ya kuzaliwa upya iliwachanganya. Baba wa familia hii jirani alisikika akisema, “Kuzaliwa mara ya pili—hilo linakuwa jambo la kidini sana kwangu!” Ungemshauri Hosea amwambie jirani yake nini ili kufafanua uhusiano wa imani na kazi ndani ya kanisa na kupitia kanisa? Alipotembelea kanisa analoshiriki rafiki yake, Shirley alipigwa na butwaa kuona msisitizo katika kanisa juu ya fedha – kupata pesa na kutoa pesa. Mfululizo wa mahubiri uliokuwa ukiendelea ulikuwa juu ya kutoa ili kupata kutoka kwa Mungu. Jambo moja ambalo Mchungaji alisema lilimfanya ajiulize kama yalikuwa mafundisho ya Biblia au la. Mchungaji alisema kwamba ikiwa mtu hayuko tayari kusaidia kanisa lake na mchungaji wake kifedha basi kuna uwezekano kabisa kwamba mtu huyo hajaokoka, na anahitaji kuchunguza upya sifa na misingi ya imani yake. Kwa maneno na sauti yenye nguvu, mchungaji alisema kwa msisitizo, “Ushahidi uko katika matendo. Kusema tu wewe ni Mkristo haitoshi; inabidi uthibitishe kwa usahihi kile unachoamini kwa jinsi unavyotenda na kile unachotoa. Naweza hata kusema kwamba ukikutana na mtu anayejiita Mkristo na huku ni bahili, pengine hajaokoka kiukweli. Kumjua Mungu ni kuwa mkarimu, hasa kifedha!” Je, ungemsaidiaje Shirley kutathmini mafundisho haya aliyoyasikia Jumapili ile alipotembelea kanisani kwa rafiki yake? Ushahidi Uko katika Matendo

3

2

Ukishaokoka, Umeokoka Milele!

James anaamini kwamba wakati fulani fundisho la “usalama wa milele” (yaani fundisho kwamba mtu anapookolewa kwa imani katika Yesu Kristo, hawezi kupotea tena) limetumika kama kichaka cha kujificha ili kutenda maovu. Kama mwalimu wa Shule ya Jumapili, James anawiwa sana na suala la “kuipa miguu na mikono imani yetu,” si kusema maneno tu bali kuishi uhalisia wa imani yetu katika matendo

3

Made with FlippingBook flipbook maker