Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 7 7
U O N G O F U & W I T O
na mtindo wa maisha wenye bidii. Akiwa amesadikishwa na maandiko kama Yakobo 2:14-26 na Waefeso 2:10, James anasisitiza kwamba tunaweza tu kuwajua wale ambao wameokoka kihalali kwa matendo yao mema na kazi zinazoonekana. Ameona kwamba baadhi ya wanaoshikilia msimamo wa “ukishaokoka, umeokoka milele” mara nyingi hawaonyeshi ile aina ya nguvu, bidii na kujitoa anayoamini kwamba Wakristo wanapaswa kuonyesha. Ametokea kuamini, hata hivyo, kwamba kiini cha mafundisho hayo ni sahihi. Msimamo wa James ni kwamba yule anayetubu na kumwamini Yesu amezaliwa mara ya pili na kupokea uzima wa milele. Hoja yake ni kwa nini wengi wanaosema wanaamini wanaonyesha dalili kidogo sana au hawaonyeshi dalili yoyote kabisa ya kuamini kwao? Kwa kiasi fulani amechanganyikiwa na amekata tamaa. Je, ungemsaidiaje James kuelewa uhusiano kati ya kukiri imani na udhihirisho wa imani yako katika maisha?
Neno Linalogeuza Sehemu ya 1
YALIYOMO
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
3
Sehemu hii inachunguza uhusiano kati ya Neno la Mungu na uwezo wake kumgeuza na kumbadilisha mtu. Katika somo hili tutajifunza namna ambavyo Injili ya Yesu Kristo ni Neno linalogeuza. Injili hii ya Yesu Kristo inayogeuza inatuongoza kwenye metanoia , yaani, kwenye toba ya kweli ya dhambi na kumgeukia Mungu katika Yesu Kristo. Zaidi ya hayo, tutaona namna ambavyo Injili hii hii inayozaa toba ndani ya mwamini pia inatusukuma kuelekea katika imani. Neno linalotuongoza kwenye toba pia linatuongoza kwenye imani ( pistis ), imani iliyo hai ambayo kwayo Mungu anamwokoa na kumkomboa mwamini na adhabu, nguvu, na uwepo wa dhambi. Lengo letu la sehemu hii ya kwanza ya Neno Linalogeuza ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno la Mungu, Neno linalogeuza, linamaanisha moja kwa moja habari njema ya wokovu kwa imani katika Yesu Kristo. Injili ya Yesu Kristo ndilo Neno linalogeuza, likiweka wazi masharti ya wokovu katika Kristo. • Neno linalogeuza huzaa toba ( metanoia ), kugeuka kutoka katika dhambi na ibada za sanamu na kuingia katika imani katika Yesu Kristo. Toba hii inajumuisha (miongoni mwa mambo mengine) badiliko la nia, huzuni ya kimungu kwa ajili ya dhambi, na kuungama dhambi mbele za Bwana na kuziacha.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
Made with FlippingBook flipbook maker