Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

7 8 /

U O N G O F U & W I T O

• Neno linalogeuza, Neno hilo linalozaa toba, linaambatana na imani iokoayo katika Yesu Kristo kama Bwana, utegemezi wa makusudi katika Yesu Kristo kuokoa na kukomboa nafsi ya mtu kutokana na adhabu, nguvu, na uwepo wa dhambi.

I. Injili ya Yesu Kristo ni Neno Linalogeuza.

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

A. Injili ya Yesu Kristo, ambayo ni nguvu ya Mungu iletayo wokovu kwa Wayahudi na Wayunani, ni neno kuhusu dhabihu ya Yesu Msalabani.

ukurasa 192  5

1. Kabla ya Msalaba , neno la wokovu lilikuja kwa sura ya taraja , yaani tumaini la kazi ya Masihi, iliyowakilishwa na damu ya wanyama waliotolewa dhabihu.

3

a. Wazo la «upatanisho» katika Agano la Kale linahusika na dhana ya kupita juu ya dhambi ambayo kwa ajili yake «ulifanyika upatanisho.» Mfumo wa dhabihu ulitazamia kwa hamu siku ambayo Mwana Kondoo halisi wa Mungu angesuluhisha mambo yote mbele za Mungu kuhusiana na dhambi na haki. b. Upatanisho unaweza kueleweka kupitia vifungu viwili muhimu katika Agano Jipya. (1) Warumi 3:25 - …ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilizotangulia kufanywa. (2) Matendo 17:30 - Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.

c. Katika zama hizi, Yesu wa Nazareti sasa amekuwa Pasaka wetu, Yule ambaye dhabihu yake ya damu msalabani ililipia gharama ya dhambi zetu. Kiuhalisia, kwa kifo chake dhambi zetu “zinafutwa,” 1 Kor. 5:7-8.

Made with FlippingBook flipbook maker