Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 7 9
U O N G O F U & W I T O
2. Baada ya Msalaba , Neno linalogeuza ni Injili ya Yesu Kristo.
a. Yesu ni Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (yaani, kwa dhabihu yake Msalabani), Yoh. 1:29.
b. Yesu alifuta kumbukumbu ya deni letu pale msalabani, pamoja na madai yote ya kisheria dhidi yetu, Kol. 2:14-15.
c. Dhabihu ya Yesu msalabani inatosha kabisa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi, Ebr. 10:11-13.
3. Yesu alikufa badala ya wanadamu wenye dhambi, akibeba katika mwili wake hatia na mashutumu yetu, 1 Pet. 2:24.
3
4. Neno linashuhudia kuhusu upeo wa kazi iliyokamilika ya Mungu katika Yesu Kristo.
a. Kazi yake ilikuwa kwa ajili ya ulimwengu wote. (1) Yohana 3:16 (2) Ebr. 2:9
b. Kazi yake pia ilikuwa kazi ya usuluhishi na ukombozi kwa wanadamu wote, 1Tim. 2:5-6.
c. Kazi yake ilikuwa kazi ya upatanisho kwa wanadamu wote. (1) 2 Kor. 5:18-21 (2) 1 Yohana 2:2
B. Uongofu unahusu Neno, si matendo.
Made with FlippingBook flipbook maker