Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
/ 8 5
U O N G O F U & W I T O
Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine yatokanayo na maudhui ya video. Neno linalogeuza ni Injili ya Yesu, inayotuongoza kwenye toba na imani, na hatimaye katika wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Kujua na kuelewa dhana hizi ni muhimu kwa ajili ya huduma na ufuasi, hasa dhana hizi za Matengenezo kuhusu sola gratia (kwa neema pekee) na sola fides (kwa imani pekee). Tafadhali jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Ili kuanza uhusiano na Mungu katika Kristo, kwa nini ni muhimu kwa mtu kushuhudia maisha mapya ndani, na sio tu mabadiliko ya nje ya mtindo wa maisha? 2. Kuna uhusiano gani kati ya Neno la Mungu katika Injili na kuokoka kwa mwamini mpya? Kwa nini ni muhimu kuamini habari njema za Kristo ili kuokolewa na Mungu? 3. Nini maana ya kibiblia ya neno metanoia ? Taja baadhi ya vipengele vya msingi vya kibiblia kuhusiana na fundisho la toba ya kibiblia. Je, inawezekana kuwepo na imani iletayo wokovu ambayo haijumuishi tendo la toba ndani yake? Elezea jibu lako. 4. Nini maana ya neno sola gratia ? Je! Neno hili linatusaidiaje kuelewa asili ya Neno linalogeuza? 5. Ni ufafanuzi gani unaotolewakuhusu sola fides ? Je, fundisho laMatengenezo ya Kanisa (“kwa neema kwa njia ya imani pekee”) linatusaidiaje kuelewa jinsi Mungu anavyogeuza roho ya mtu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo? 6. Orodhesha vitumaalumvinavyohusishwa na ushuhuda wa kitume kuhusu Yesu Kristo. Je, sisi kama waamini tunapaswa kuupokeaje ushuhuda huu walioutoa kwa habari ya maisha, kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo? 7. Je, ni nyakati zipi tatu zinazohusishwa na ukombozi na uweza wa Mungu wa kugeuza maisha ya mtu kwa njia ya Yesu Kristo? Je, Mungu anaweza kuokoa katika awamu moja, na mwamini akapotea katika awamu nyingine? Eleza. 8. Kwa nini ni muhimu kutoifikiria kamwe toba na imani kama kazi ambayo mwamini hufanya ili kupata kibali cha Mungu na msamaha wake?
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 194 8
3
Made with FlippingBook flipbook maker