Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
8 6 /
U O N G O F U & W I T O
Neno Linalogeuza Sehemu ya 2
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Katika sehemu hii tunatumai kuonyesha jinsi Injili ya Yesu Kristo, Neno hili la Mungu linalogeuza, inavyozalisha ishara zinazothibitisha msamaha wa Mungu na uwepo wa nguvu za Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. Neno linalogeuza hutokeza ishara za ndani za maisha ambazo hutumika kama ushahidi kuonyesha mabadiliko ya mwongofu mpya katika Yesu Kristo. Mambo hayo yanajumuisha kumjua Mungu kama Baba wa mbinguni, uzoefu mpya wa maombi, uwazi kwa Neno la Mungu, na utayari wa kufuata uongozi wa ndani wa sauti ya Yesu. Vivyo hivyo, mwamini katika Injili ya Yesu anadhihirisha ishara za nje, ikiwa ni pamoja na kujitambulisha na kuwa na ushirika na watu wa Mungu, kuonyesha tabia mpya na mtindo mpya wa maisha unaomfanania Kristo na upendo kwa waamini wengine, pamoja na kuonyesha shauku ya kuona waliopotea wakirudi kwa Kristo. Lengo letu la sehemu hii ya pili ya Neno Linalogeuza ni kukuwezesha kuelewa, kukariri, na kujadili ukweli ufuatao: • Neno linalogeuza ni nguvu yenye uweza, inayozaa upya maisha halisi ya Mungu katika moyo na maisha ya Mkristo, yanayodhihirishwa ndani na nje kwa ishara (ushahidi) wa utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. • Neno hili linalogeuza watu na linalozaa uzima hutokeza ishara za ndani zinazotoa uhakikisho wa ndani wa utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Ishara hizi ni pamoja na kumjua Mungu kama Baba wa mbinguni, uzoefu mpya wa maombi, uwazi kwa Neno la Mungu, na utayari wa kufuata uongozi wa ndani wa sauti ya Yesu kama Mchungaji wa maisha ya mwamini. • Neno la Mungu pia hutokeza ishara za nje ambazo kila Mkristo wa kweli hudhihirisha, zikijumuisha ushirika wa hadharani na kujitambulisha na watu wa Mungu, udhihirisho wa shauku mpya, maadili na mtindo mpya wa maisha kupitia tabia mpya inayomfanania Kristo, upendo kwa waamini wengine, na shauku inayokua ya kuona waliopotea wakiokolewa na kurudi kwa Yesu Kristo.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
3
Made with FlippingBook flipbook maker