Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

/ 8 7

U O N G O F U & W I T O

I. Neno Lile Ligeuzalo Linatokeza Ishara za Ndani za Maisha Ambazo Hutumika kama Ushahidi wa Kuonyesha Mabadiliko Yetu Katika Yesu Kristo.

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

ukurasa 194  9

A. Ishara moja ni kuongezeka kwa uhakikisho wa ndani kwamba Mungu amekuwa Baba wa mbinguni wa mwamini mpya.

2 Wakorintho 13:5 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.

1. Uzima wa milele ni kumjua Baba kupitia Mwanawe , Yesu Kristo, Yohana 17:3.

2. Hii lazima iwe kazi ya Mungu pekee , kwani hakuna awezaye kumjua Mungu bila kazi ya Yesu, Mt. 11:27.

3. Roho hushuhudia katika roho ya mwamini kwamba yeye ni wa Baba, Rum. 8:16-17.

3

4. Wale walio wa Mungu watakua katika imani inayoongezeka daima ya kwamba wao ni wa Bwana , kwamba Mungu na Baba wa Yesu Kristo ndiye Mungu wao, 1 Yoh. 3:19-24.

B. Ishara nyingine ya ndani ya uongofu wa kweli ni uzoefu wa kuzungumza na Mungu kwa njia ya maombi.

1. Roho Mtakatifu huja na kukaa ndani ya mwamini mpya kwa imani , na uwepo wake ndani ya Mkristo huzalisha hamu mpya ya kuwasiliana na Mungu. Roho Mtakatifu humjaza Mkristo na kumwezesha kuomba na kumwabudu Mungu.

a. Mjazwe kwa Roho Mtakatifu, Efe. 5:18-19.

Made with FlippingBook flipbook maker