Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

8 8 /

U O N G O F U & W I T O

b. Shukuruni kwa kila jambo, kwa kuwa haya ni mapenzi ya Mungu kwenu, 1 Thes. 5:16-18.

2. Roho Mtakatifu huimarisha maombi ya ndani ya Mkristo kwa njia za kina za kiroho, Rum. 8:26-27.

3. Sisi tuliookoka tunalia “Aba, Baba!” (Kiaramu, “ papa !”) mioyoni mwetu, tukimlilia Mungu, Baba yetu atutimizie mahitaji yetu, Rum. 8:15.

C. Ishara nyingine ya ndani ya uongofu ni uwazi na njaa ya Neno la Mungu .

1. Kama watoto wachanga waliozaliwa, waamini wa kweli hutamani maziwa ya Neno la Mungu, chanzo cha nguvu na lishe yao, 1 Pet. 2:2.

3

2. Huduma ya kufundisha ya Roho Mtakatifu huzalisha viwango vipya vya utambuzi, njaa, na bidii kwa ajili ya Neno la Mungu.

a. 1 Kor. 2:15

b. 1 Yohana 2:27

c. Yohana 16:12-15

3. Kupitia kujilisha Neno la Mungu, mwamini huongezeka katika ufahamu wa Kristo , 2 Tim. 1:12.

Made with FlippingBook flipbook maker