Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

9 0 /

U O N G O F U & W I T O

2. Akiwa amesafishwa na Neno liletalo uzima, mwamini mpya anakaliwa na Roho Mtakatifu ndani yake na kupewa asili mpya ambayo “inafanywa upya katika ufahamu kwa mfano wa Muumba wake.”

a. Kol. 3:9-11

b. Efe. 2:19

3. Baada ya kuzaliwa katika familia ya Mungu, waamini wapya wanakuwa washirika wa nyumba ya Mungu na kuwa na hamu ya kukua na kuwa pamoja na waamini wengine, Gal. 3:26-28.

4. Wale ambao wameongoka kweli kweli hawatapuuza umuhimu wa ushirika, bali watajitambulisha na kushirikiana pamoja na watu wa Mungu kama watu wao wapya , Ebr. 10:24-25.

3

5. Wale wanaokataa ushirika na mwili wa Kristo hujidhihirisha kuwa aidha wana nia ya kiulimwengu, au wao si mali ya Mungu kabisa, 1 Yoh. 2:19.

B. Wale ambao wamelipokea Neno liletalo badiliko watadhihirisha zaidi na zaidi tabia za Yesu katika maisha yao.

1. Kusudi la Mungu ni kuwafanya watoto wake wote wafanane na Mwanawe .

a. Warumi 8:28-29

b. 2 Wakorintho 3:18

Made with FlippingBook flipbook maker