Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
100
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Kiambatisho cha 3 Tunaamini: Ukiri wa Imani ya Nikea (8.7.8.7. meter*) Mch. Dkt. Don L. Davis, 2007. Haki Zote Zimehifadhiwa.
* Wimbo huu umechukuliwa kutoka kwenye Imani ya Nikea, na kuwekwaa kwenye mita 8.7.8.7., ikimaanisha kuwa unaweza kuimbwa kwa sauti zenye mita sawa, kama vile: Joyful, Joyful, We Adore Thee; I Will Sing of My Redeemer; What a Friend We Have in Jesus; Come, Thou Long Expected Jesus
Baba Mungu Mwenyezi anatawala, Muumba wa dunia na mbingu. Vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, viliumbwa na yeye, vilitolewa na yeye!
Tunamwamini Yesu Kristo, Bwana, Mwana pekee wa Mungu, Aliyezaliwa, hajaumbwa, pia, yeye na Baba yetu Mungu ni mmoja!
Aliyezaliwa kutoka kwa Baba, sawa, kwa asili, kama vyote, Mungu na Nuru; Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na katika yeye vitu vyote vilihuishwa. Ambaye kwa ajili yetu sisi sote, kwa ajili ya wokovu wetu, alishuka kutoka mbinguni kuja duniani, Akifanyika mwili kwa uwezo wa Roho, na kwa kuzaliwa kwa Bikira Maria. Ambaye kwa ajili yetu pia, alisulubishwa, kwa utawala na mkono wa Pontio Pilato, Aliteseka, akazikwa, lakini siku ya tatu alifufuka. Kulingana na Maandiko Matakatifu yote yaliyotukia yalikusudiwa kuwa. Alipaa juu kwenda mkono wa kuume wa Mungu, mbinguni ameketi katika utukufu. Kristo atakuja tena katika utukufu kuwahukumu wote walio hai na waliokufa. Utawala wa Ufalme wake hautakoma kamwe, kwa kuwa atatawala akiwa Kichwa. Tunamwabudu Mungu, Roho Mtakatifu, Bwana na Mtoa-Uzima anayejulikana; Ambaye pamoja na Baba na Mwana hutukuzwa, Ambaye aliwahi kunenwa na manabii. Na tunaamini katika Kanisa moja la kweli, watu watakatifu wa Mungu milele, La ulimwengu katika upeo na upana wake, lililojengwa juu ya mstari wa Mitume! Tunautambua ubatizo mmoja, kwa ondoleo la dhambi zetu, Na tunatazamia Ufufuo, kwani wafu wataishi tena. Tunatazamia siku zisizo na mwisho, maisha ya Enzi safi inayokuja, Wakati Utawala wa Kristo utakapokuja duniani, mapenzi ya Mungu yatatimizwa! Sifa kwa Mungu, na kwa Kristo Yesu, kwa Roho-Bwana wa Utatu! Tunakiri mafundisho ya kale, tukishikamana na Neno takatifu la Mungu!
*Wimbo/shairi hili ni la Kingereza na limmechukuliwa kutoka kwenye Imani ya Nikea.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software