Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

104

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Hapo Zamani za Kale, muendelezo

wake kwa ajili ya kuurejesha, kuangamiza uovu mara moja na kwa zote, na kuanzisha jamii ya watu ambao Bingwa wao atakuja kuuthibitisha utawala wake katika ulimwengu huu kwa mara nyingine tena. Kwa hiyo, aliinua watu ambao Mtawala angetoka kwao. Na kwa hivyo, kupitia kwa Nuhu, anaokoa ulimwengu kutoka kwa uovu wake wenyewe, kupitia kwa Ibrahimu, anachagua ukoo ambao kupitia huo mzao angekuja. Kupitia Isaka, anaendeleza ahadi aliyomuahidi Ibrahimu, na kwa njia ya Yakobo (Israeli) analisimamisha taifa lake, akitambulisha kabila ambalo atatoka (Yuda). Kupitia Musa, anawakomboa walio wake kutoka katika ukandamizaji na kuwapa sheria yake ya agano, na kupitia Yoshua, anawaleta watu wake katika nchi ya ahadi. Kupitia waamuzi na viongozi, anawasimamia watu wake, na kupitia kwa Daudi, anafanya agano la kuleta Mfalme kutoka kwa ukoo wao ambaye atatawala milele. Licha ya ahadi yake, mara kwa mara watu wake wanashinwa kutimiza agano lake. Usumbufu wao na ukaidi wao endelevu kwa Bwana hatimaye unapelekea kwenye hukumu ya taifa, uvamizi, kupinduliwa, na utumwa. Kwa rehema, anakumbuka agano lake na kuruhusu mabaki kurudi - kwa maana ahadi na hadithi hazikufikia utimilifu. Takribani miaka mia nne ya ukimya ilipita. Hata hivyo, katika utimilifu wa wakati, Mungu alitimiza ahadi yake ya agano kwa kuingia kwa njia ya mwili katika ulimwengu huu mwovu, wenye mateso, na uliotengwa. Katika nafsi ya Yesu wa Nazareti, Mungu alishuka kutoka mbinguni na kuishi kati yetu, akionyesha utukufu wa Baba, akitimiza matakwa ya sheria ya maadili ya Mungu, na kuonyesha nguvu za Ufalme wa Mungu katika maneno yake, kazi zake, na kutoa pepo. Pale msalabani alichukua uasi wetu, akaharibu kifo, akamshinda shetani, na akafufuka siku ya tatu ili kurejesha uumbaji kutoka kwenye Anguko, kukomesha dhambi, maradhi, na vita, na kuwapa watu wote wanaoshikilia wokovu wake uzima usio na mwisho. Akiwa amepaa kwenda mkono wa kuume wa Baba, Bwana Yesu Kristo amemtuma Roho Mtakatifu ulimwenguni, na kuunda jamii mpya ya watu ambao ni Wayahudi na Wamataifa, yaani, Kanisa. Wakiwa wametumwa chini ya utawala wake, wanashuhudia kwa maneno na matendo injili ya upatanisho kwa viumbe vyote, na watakapomaliza kazi yao, atarudi katika utukufu na kukamilisha Ambaye, kama Bingwa, alishuka kutoka mbinguni, katika utimilifu wa wakati, na kushinda kwa njia ya Msalaba. Na, hivi karibuni kabisa, atarudi katika ulimwengu huu na kufanya mambo yote kuwa mapya.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software