Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipinidi cha 1 Utangulizi Kutambua Eneo lako la Utumishi katika Jumuiya ya Kiagano ya Mungu
Viongozi wa kweli ni wachache. Watu na vikundi huwatafuta kila wakati. Katika Biblia yote, Mungu anatafuta viongozi pia. “Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake” (1 Sam. 13:14). “Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.” (Yer. 5:1). “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka” (Eze. 22:30). Biblia inatuonyesha kwamba Mungu anapompata mtu aliye tayari kuongoza, kujitoa katika ufuasi kamili na kuchukua jukumu kwa ajili ya wengine, mtu huyo anatumiwa kwa viwango vya juu. Viongozi wa aina hii bado huwa na mapungufu na kasoro, lakini pamoja na hayo, wanafanyika viongozi wa kiroho. Hivyo ndivyo walivyokuwa watu kama Musa, Gideoni, na Daudi. Na katika historia ya Kanisa, Martin Luther, John Wesley, Adoniram Judson, William Carey, na wengine wengi [ wakiwemo Debora, Esta, Mariamu, na katika Kanisa Sojourner Truth, Elisabeth Elliott, Mama Theresa, na Aimee Semple McPherson , italiki ni yangu]. Kuwa kiongozi katika Kanisa daima kumekuwa kukihitaji nguvu na imani izidiyo ile ya mwanadamu wa kawaida. Kwa nini hitaji letu la viongozi ni kubwa, na viongozi waliopo ni wachache mno? Kila kizazi kinakabiliwa na mahitaji makubwa ya uongozi wa kiroho, na huwapata wachache wanaojitokeza kuhudumu.
~ J. Oswald Sanders. Spiritual Leadership . Toleo la 2. Chicago: Moody Press, 1994. uk. 18.
I. Theolojia Simulizi na Hadithi ya Kutoka: Kutafuta Mbinu Inayoaminika ya Kitheolojia ili Kuelewa Wito wa Mungu.
Musa na Wito wa Mungu Kut. 3:1-10 – Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. 3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. 4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. 5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana
11
Made with FlippingBook Digital Publishing Software