Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Viambatisho

119

Kiambatisho cha 16 Mapokeo (Paradosis) Mch. Dkt. Don L. Davis na Mch. Terry G. Cornett

Ufafanuzi wa Strong

Paradosis. Uenezaji, yaani (kiuhalisia) agizo; hasa, sheria ya mapokeo ya Kiyahudi

Ufafanuzi wa Vine

lnadokeza “mapokeo,” na kwa hiyo, kwa lugha ya picha, (a) “mafundisho ya marabi,” . . . (b) “mafundisho ya kitume,” . . . ya maagizo kuhusu mikusanyiko ya waumini, ya mafundisho ya Kikristo kwa ujumla . . . ya maelekezo kuhusu mwenendo wa kila siku.

1. Dhana ya mapokeo katika Maandiko kimsingi ni chanya.

Yeremia 6:16 - Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo. (rej. Kut. 3:15; Amu. 2:17; 1 Fal. 8:57-58; Zab. 78:1-6). 2 Nyakati 35:25 - Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote waume kwa wake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hata leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika maombolezo. (rej. Mwa. 32:32; Amu. 11:38-40). Yeremia 35:14-19 - Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza mimi. 15 Pia naliwapeleka watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiamka mapema na kuwapeleka, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiwafuate miungu mingine, ili kuwatumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza. 16 Basi, kwa kuwa wana wa Yonadabu, mwana wa Rekabu,

Made with FlippingBook Digital Publishing Software