Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

120

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Mapokeo, mwendelezo

wameitimiza amri ya baba yao aliyowaamuru, lakini watu hawa hawakunisikiliza mimi; 17 kwa sababu hiyo, asema Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli; Tazama nitaleta juu ya Yuda, na juu ya wenyeji wote wa Yerusalemu, mabaya yote niliyoyatamka juu yao; kwa sababu nimesema nao, wasinisikilize; nimewaita, wala hawakuniitikia. 18 Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru; 19 basi, kwa sababu hiyo, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu hata milele

1 “Waprotestanti wote wanasisitiza kwamba mapokeo haya lazima yajaribiwe dhidi ya Maandiko na hayawezi kamwe kuwa na mamlaka huru ya kitume juu au kando ya Maandiko.” (J. Van Engen, “Tradition,” Evangelical Dictionary of Theology, Walter Elwell, Gen. ed.) Tungeongeza kwamba Maandiko yenyewe ndiyo “mapokeo yenye mamlaka” ambayo kwayo mapokeo mengine yote yanapimwa. Tazama

2. Mapokeo ya kimungu ni jambo zuri ajabu, lakini si mapokeo yote ni ya kimungu.

Mapokeo yoyote lazima yapimwe kwa uaminifu wake kwa Neno la Mungu na manufaa yake katika kuwasaidia watu kudumisha utii kwa kielelezo na mafundisho ya Kristo. 1 Katika Injili, mara nyingi Yesu anawakemea Mafarisayo kwa kuanzisha mapokeo ambayo yanabatilisha badala ya kuunga mkono amri za Mungu.

Marko. 7:8 - Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu

Wakolosai 2:8 - Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

3. Bila ujazo wa Roho Mtakatifu, na kule kujengwa tunakojengwa mara zote na Neno la Mungu, bila shakamapokeo yatapelekea kwenye taratibu mfu. Wale walio wa rohoni wamejazwa na Roho Mtakatifu, ambaye uwezo wake na uongozi pekee huwapa watu binafsi na kusanyiko hisia ya uhuru na uchangamfu katika yote wanayofanya na kuamini. Hata hivyo, wakati desturi na mafundisho ya mapokeo yoyote hayajajazwa kabisa na nguvu za Roho Mtakatifu na Neno la Mungu, mapokeo yanapoteza ufanisi wake, na yanaweza kuwa kinyume na ufuasi wetu katika Yesu Kristo.

“Kiambatisho A, Vyanzo vya Mapokeo: Ngazi

Tatu za Mamlaka ya Kikristo,” mwishoni mwa hati hii.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software