Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
128
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Uandishi Sahihi wa Kazi yako, mwendelezo
Ukurasa wa “Kazi Zilizonukuliwa” unapaswa kuwekwa mwishoni mwa karatasi yako. Ukurasa huu:
Kuunda Ukurasa wa Kazi Zilizonukuliwa
• huorodhesha kila chanzo ulichonukuu kwenye karatasi yako • Huwa katika mpangilio wa alfabeti kwa jina la mwisho la mwandishi • Hujumuisha tarehe ya kuchapishwa na taarifa kuhusu mchapishaji
Kanuni zifuatazo za uundaji zinapaswa kufuatwa:
1. Kichwa
Kichwa “Kazi Zilizonukuliwa” kinapaswa kutumiwa na kuwekwa juu kabisa ya ukurasa.
2. Yaliyomo
Kila marejeo yanapaswa kuorodhesha:
• jina kamili la mwandishi (jina la mwisho kwanza) • tarehe ya kuchapishwa • kichwa na taarifa yoyote maalum (toleo lililorekebishwa, toleo la 2, kuchapishwa tena) iliyochukuliwa kutoka kwa jalada au ukurasa wa kichwa inapaswa kuzingatiwa. • mji ambapo ni makao makuu ya mchapishaji ikifuatiwa na koloni na jina la mchapishaji
3. Muundo wa Msingi
• Kila kipande cha taarifa kinapaswa kutengwa kwa nukta.
• Mstari wa pili wa rejeleo (na mistari yote ifuatayo) inapaswa kuingizwa ndani.
• Vichwa vya vitabu vinapaswa kupigwa mstari (au kuwekwa kwenye italic).
• Vichwa vya makala vinapaswa kuwekwa katika nukuu.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software