Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Viambatisho
127
Kiambatisho cha 17 Uandishi Sahihi wa Kazi yako Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua na Kutoa Sifa mahali Sifa inapohitajika The Urban Ministry Institute Ulaghai ni kutumia mawazo ya mtu mwingine kana kwamba ni yako bila kumtambua na kumpa sifa ifaayo mhusika. Katika kazi ya kitaaluma kuiba mawazo ya mtu ni kosa kama tu ilivyo kuiba mali yake. Mawazo haya yanaweza kutoka kwa mwandishi wa kitabu, makala uliyosoma, au kwa mwanafunzi mwenzako. Njia ya kuepuka ulaghai ni kutumia kwa uangalifu “vidokezo” (tanbihi n.k.) na sehemu ya “Kazi Zilizonukuliwa” ili kuwasaidia watu wanaosoma kazi yako kujua wakati gani ulitumia wazo lako, na ni wakati gani uliazima kutoka kwa mtu mwingine.
Kuepuka Ulaghai
Rejeleo la nukuu linahitajika wakati wowote unapotumia mawazo au maelezo yaliyotoka kwenye kazi ya mtu mwingine.
Kwa kutumia Marejeleo ya Nukuu
Marejeleo yote ya nukuu yanajumuisha sehemu mbili:
• Vidokezo kwenye karatasi yako vilivyowekwa karibu na kila nukuu iliyotoka kwenye chanzo cha nje.
• Ukurasa wa “Kazi Zilizonukuliwa” mwishoni mwa karatasi au project yako ambayo inatoa taarifa kuhusu vyanzo ambavyo umetumia
Kuna aina tatu za msingi za vidokezo: vidokezo vya mabano na tanbihi. Hapa The Urban Ministry Institute, tunapendekeza kwamba wanafunzi watumie vidokezo vya mabano. Vidokezo hivi vinatoa jina la mwisho la mwandishi, tarehe ambayo kitabu kilichapishwa, na nambari za ukurasa ambapo ulipata habari. Kwa mfano: Katika kujaribu kuelewa maana ya Mwanzo 14:1-24, ni muhimu kutambua kwamba katika hadithi za Biblia “mahali ambapo mazungumzo yanatambulishwa kwanza patakuwa muhimu katika kufunua tabia ya mzungumzaji . . .” (Kaiser na Silva 1994, 73). Hii ni kweli kuhusu tabia ya Melkizedeki ambaye anazungumza maneno ya baraka. Utambulisho huu wa Melkizedeki kama kishawishi chanya cha kiroho unaimarishwa na ukweli kwamba yeye ndiye Mfalme wa Salemu, kwa kuwa Salemu inamaanisha “salama, kwenye amani” (Wiseman 1996, 1045).
Kutumia Vidokezo kwenye Karatasi Yako
Made with FlippingBook Digital Publishing Software