Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Viambatisho
153
Kiambatisho cha 35 Kuteseka Kwa ajili ya Injili Gharama ya Ufuasi na Uongozi wa Utumishi Mch. Dkt. Don L. Davis
Kuikubali Injili na kutoionea haya (Rum. 1:16) ni kubeba unyanyapaa na aibu ya yeye aliyewaita katika utumishi (2 Tim. 3:12). Kimsingi, hii inaweza kumaanisha kupoteza faraja, wepesi, na hata maisha yenyewe (Yn. 12:24-25). Kama mabalozi wa Kristo, tunaowasihi wanaume na wanawake waje kwake, hatupaswi hata kuyahesabu maisha yetu kuwa ya thamani kwetu, bali tuwe tayari daima kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya Habari Njema (Mdo. 20:24). Mitume wote wa Kristo walistahimili matusi, makaripio, viboko, na kukataliwa na maadui wa Bwana wao (taz. 2 Kor. 6, 11). Kila mmoja wao alitia muhuri mwito wake kwa Kristo na kwa fundisho lake kwa damu yake uhamishoni, katika mateso, na kifo cha imani. Zilizoorodheshwa hapa chini ni hatima za mitume kulingana na hadithi za mapokeo.
• Mathayo aliuawa kwa kukatwa kichwa kwa upanga katika jiji la mbali la Ethiopia.
• Marko aliishia Alexandria, baada ya kuburutwa kikatili katika barabara za jiji hilo.
• Luka alitundikwa juu ya mzeituni katika nchi ya Ugiriki.
• Yohana aliwekwa kwenye pipa ya mafuta yaliyokuwa yakichemka, lakini aliepuka kifo kwa njia ya kimuujiza, na baadaye alifukuziwa kule Patmo.
• Petro alisulubishwa huko Rumi akiwa amepinduliwa, na kichwa chake kikiwa chini.
• Yakobo , mkubwa, alikatwa kichwa huko Yerusalemu.
• Yakobo , mdogo, alitupwa kutoka kwenye kilele kirefu cha hekalu, na kisha akapigwa hadi kufa kwa rungu.
• Bartholomayo alichunwa ngozi akiwa hai..
• Andrea alifungwa msalabani, ambapo aliwahubiria watesi wake hadi akafa.
• Thomaso alirushiwa mkuki huko Coromandel India ya Mashariki.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software