Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

154

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

Kuteseka Kwa ajili ya Injili, mwendelezo

• Yuda aliuawa kwa kupigwa mishale.

• Matthia alipigwa kwa mawe hadi kifo na baadaye akakatwa kichwa .

• Barnaba mtume wa Mataifa alipigwa kwa mawe hadi kufa katika mji wa Salonica.

• Paulo , baada ya mateso mbalimbali, hatimaye alikatwa kichwa huko Roma na Mfalme Nero

Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizungukazunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

~ Waebrania 11:32-40

Made with FlippingBook Digital Publishing Software