Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
162
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
Kiambatisho cha 41 Wajibu wa Wanawake katika Huduma Mch. Dkt. Don L. Davis
Ingawa ni wazi kwamba Mungu ameweka utaratibu uliopangwa wazi wa wajibu nyumbani, ni wazi vile vile kwamba wanawake wameitwa na kupewa karama na Mungu, wakiongozwa na Roho wake mwenyewe kuzaa matunda yanayostahili wito wao katika Kristo. Katika Agano Jipya lote, amri zinaelekezwa haswa kwa wanawake kunyenyekea, na kitenzi fulani cha Kiyunani hupotasso , kikitokea mara kwa mara kikimaanisha “kuweka chini” au “kunyenyekea” (taz. 1 Tim. 2:11). Neno pia lililotafsiriwa katika neno letu la Kiingereza “subjection” linatokana na mzizi mmoja. Katika mazingira kama haya tafsiri hizi za Kiyunani hazipaswi kueleweka kwa njia yoyote isipokuwa kama maonyo chanya kuelekea mfumo wa Mungu ulioundwa kwa ajili ya nyumba, ambapo wanawake wameagizwa kujifunza kwa utulivu na unyenyekevu, kuamini na kufanya kazi ndani ya mpango wa Bwana mwenyewe. Hata hivyo, utaratibu huu wa unyenyekevu wa mwanamke nyumbani, haupaswi kutafsiriwa vibaya kana kwamba unamaanisha wanawake wamekataliwa kuzitumia karama zao chini ya uongozi wa Roho. Hakika, ni Roho Mtakatifu kwa njia ya majaliwa ya neema ya Kristo ambaye hugawa karama kama apendavyo, kwa ajili ya kulijenga Kanisa (1 Kor. 12:1-27; Efe. 4.1 16). Karama hizi hazitolewi kwa waamini kwa vigezo vya jinsia; kwa maneno mengine, hakuna dalili kutoka katika Maandiko kwamba baadhi ya karama ni kwa ajili ya wanaume tu, na nyingine ni kwa ajili ya wanawake tu. Kinyume chake, Paulo anathibitisha kwamba Kristo alitoa karama kama matokeo ya moja kwa moja ya ushindi wake binafsi dhidi ya shetani na wafuasi wake (taz. Efe. 4:6 na kuendelea). Hili lilikuwa ni chaguo lake binafsi, alilopewa na Roho wake kwa yeyote amtakaye (rej. 1Kor. 12:1-11). Katika kuthibitisha huduma ya wanawake tunathibitisha haki ya Roho kuwa mbunifu mtendaji mkuu katika watakatifu wote kwa ajili ya ustawi wa wote na upanuzi wa Ufalme wake, kama yeye aonavyo inafaa, na si lazima kama sisi tunavyoamua (Rum. 12:4-8; 1 Pet. 4:10-11). Zaidi ya hayo, usomaji makini wa Maandiko kwa ujumla unaonyesha kwamba mpangilio alioufanya Mungu kwa nyumba hakuathiri kwa vyovyote kusudi lake kwa wanaume na wanawake kumtumikia Kristo wakiwa wanafunzi na watenda kazi pamoja, chini ya uongozi wa Kristo. Fundisho la wazi la Agano Jipya la Kristo kama kichwa cha mwanamume, na mwanamume cha
Made with FlippingBook Digital Publishing Software