Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 3 : Wito wa Utakatifu
35
hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa Bwana alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.
3. Kutolewa kwa Torati Sinai: Agano la Mungu na watu wake , Kut. 19:3-6 – Musa akapanda kwa Mungu, na Bwana akamwita toka mlima ule, akisema, “Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno haya; 4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.”
a. Utambulisho wao na jumuiya yao wenyewe
b. Nidhamu, utaratibu, na utawala wao wenyewe
c. Hatima mpya: watu wa Masihi wakitoa ushahidi kwa mataifa yanayowazunguka kuhusu uaminifu wa agano la Mungu.
, hagios Neno linalotokana na mzizi mmoja na hagnos (hupatikana katika hazo , “kutoa heshima ya hali ya juu”), kimsingi humaanisha “kutengwa” (miongoni mwa Wayunani, kuwekwa wakfu kwa miungu), na kwa hiyo, katika Maandiko katika maana yake ya kiadili na kiroho, kutengwa na dhambi na hivyo kuwekwa wakfu kwa Mungu, takatifu. (a) Linamwelezea Mungu (kama “Mtakatifu” kabisa, katika usafi wake, ukuu na utukufu wake): Baba k.m., Lk. 1:49; Yn. 17:11; 1 Pet. 1:15, 16; Ufu. 4:8; Ufu. 6:10; Mwana, k.m., Lk. 1:35; Mdo. 3:14; Mdo 4:27, 30; 1 Yoh. 2:20; Roho , k.m., Mt. 1:18 na mara nyingi katika Injili zote, Matendo, Warumi, 1 na 2 Wakorintho, Waefeso, 1 Wathesalonike; pia katika 2 Tim. 1:14; Tit. 3:5; 1 Pet. 1:12; 2 Pet. 1:21; Yud. 1:20. (b) Linatumika kwa watu na vitu (tazama hapa chini) kwa kadiri wanavyojitoa kwa Mungu. Kwa hakika sifa yoyote inayohusishwa na Mungu, mara nyingi
Made with FlippingBook Digital Publishing Software