Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 3 : Wito wa Utakatifu
39
1 Pet. 1:14-16 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16 kwa maana imeandikwa, “Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu”
D. Ufahamu wa kipekee kwa viongozi wa kiroho: Je, kiongozi ambaye ameitwa kuwahudumia watu watakatifu wa Mungu anapaswa kuwa mtakatifu (aliyetengwa) kiasi gani?
1. Mashaka na vikwazo vya awali vya mtu aliyeitwa haviwezi kubatilisha au kuzuia wito wa Mungu.
a. Petro, Lk. 5:8
b. Musa, Kut. 4:13
c. Yeremia, Yer. 1:6
d. Yona, Yon. 1:2-3 – “Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu”. 3 Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana.
e. Isaya, Isa. 6:1-8
2. Mungu anaweza kumpa mwanamume au mwanamke mtumishi wake chochote anachohitaji ili kukamilisha kazi yake, ama kabla au wakati wa utumishi.
a. Upaji wa awali, 1 Tim. 3:2; Mdo. 6:3
b. Wakati wa kuwekwa wakfu, 1 Tim. 4:14; 2 Tim. 1:6
c. Katika wakati wa kazi (utumishi), Flp. 4:13
Made with FlippingBook Digital Publishing Software