Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
42
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
2. Wito wa utakatifu ni wito wa kujitenga na uchafu na mweneno mchafu wa jamii ya mijini.
3. Wito wa utakatifu ni wito wa kudhihirisha tabia takatifu ya Mungu katikati ya jamii za mijini; bila hali ya kuwa wakfu kiasi hiki, hatuwezi kukuza uhusiano na Mungu.
4. Wito wa utakatifu ni wito wa kuikabili jamii ya mijini na ukweli wa Ufalme wa Mungu.
B. Kuhusianisha somo na maisha yako
1. Je, umetambua kwamba wewe u mali ya Mungu kabisa sasa, roho, nafsi, na mwili, ili afanye ndani yako na kupitia wewe lolote analotaka? (1 Kor. 3:16-17; 6:18-20).
2. Je, unahisi wito wa ndani wa kutengwa zaidi kwa Bwana kwa ajili ya kazi ya huduma? Je, umewashirikisha viongozi wako juu ya wito huu wa ndani?
3. Ni nini maishani mwako kinachoingilia wito wako wa kuwa mtakatifu na aliyetengwa kwa makusudi ya Bwana? Unahitaji kuacha, kuepuka, kuweka chini ama kulikimbia jambo gani? Je, kuna dhambi za siri zinazohitaji umakini wako wa haraka na toba?
4. Je, kuna maeneo fulani ya maisha yako ambayo hujaweza kuwa na nidhamu nayo, jambo linalokufanya uvutwe mara kwa mara katika mfumo wa akili na mtindo wa maisha wa kidunia? 1 Tim. 4:7-8
5. Je, unawezaje kupata maarifa na maandalizi ili uweze kufuata utakatifu (kuwa wakfu) kwa Mungu katika Kristo katika kila eneo la maisha yako? Zab. 139:23-24
Made with FlippingBook Digital Publishing Software