Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Kipindi cha 4 Wito wa Uhuru Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Uhuru

Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

~ Wagalatia. 5:1

Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.

~ Kutoka 20:2

Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”

~ Yohana 8:31-32

Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. 36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli

~ Yohana 8:35-36

Ishini kama watu huru; lakini msiutumie uhuru wenu kuuficha ubaya,bali ishini kama watumishi wa Mungu.

~ 1 Petro 2:16 (BHN)

I. Kuelewa Wito Halisi kama Wito wa Uhuru

Umuhimu wa Uhuru katika Maono ya Kikristo

Uhuru sio kipengele kimoja katika maisha ya Kikristo. Sio moja ya sura zake. Haujitokezi kwa bahati nasibu, au kulingana na mazingira, au kwa matukio. Kwenye baadhi ya mazingira, kiasi ndicho kinachoakisi kazi ya imani, katika mazingira mengine uaminifu, katika mazingira mengine ni haki tu, na mengine huruma nyingi. Hata hivyo, uhuru hauko hivyo. Wenyewe si sehemu au kipengele cha kielelezo cha maisha ya Kikristo. Uhuru ndio maisha ya Kikristo. Uhuru upo nje ya orodha ya sifa njema. Si moja ya matunda ya Roho. Ni msingi ambao juu yake vingine vyote vinaweza kujengwa. Uhuru ndio mazingira yanayowezesha vitu vyote kukua na kuendelea. Ndio tafsiri na mantiki ya matendo yote. Ndio uelekeo

45

Made with FlippingBook Digital Publishing Software