Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
46
Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa
wa vyote. Ni hali ya maisha yote ya Kikristo. Kwa hivyo, uhuru, si mojawapo ya vipengele katika maadili au tabia ya Kikristo. Bila huo pasingekuwa na maadili. Maisha ya Kikristo yamewekwa ndani yake. Tena uhuru si mtazamo ambao tunaweza kuuvaa au kuutupilia mbali tupendavyo. Tumezoea kutoweka uhuru katika fikra zetu za Kikristo kiasi kwamba haingii akilini kwamba ni hali ambayo kila kitu kinajengwa juu yake. Tuko tayari kujishutumu wenyewe kwa kutokuwa na haki au upendo. Lakini huwa hatuna ndoto ya kuhoji ukosefu wetu wa uhuru au kuuliza ikiwa tunaudhihirisha katika jumla ya maisha yetu. Ikiwa sisi ni wanatheolojia, tunaweza kusema kwamba hali hii imetengenezwa kwa ajili yetu. Tuko huru kwa sababu tumewekwa huru. Uhuru umepatikana. Umetolewa. Tumekuwa huru. Hakuna namna ya kuligeuza hili. Uhuru umekuwa zaidi ya kipengele cha muhimu katika maisha na asili yangu. Kwa nini, basi, niwe na wasiwasi? Ni sehemu ya asili mpya ambayo imewekezwa kwangu. Siwezi kuipoteza kwa kuwa imetolewa kwangu kwa neema. . . . . . Sasa ujumbe huu umepata nafasi ndogo sana katika mafundisho ya Kanisa kiasi kwamba hatupati hata chembe ya kumbukumbu yake katika katekisimu zetu, wala hakuna uchunguzi wowote wa maisha ya Kikristo kwa misingi ya uhuru. Miongozo mingi ya maadili ama hupuuza uhuru, au huuweka kwa makusudi miongoni mwa sifa njema (kitu ambacho mtume Paulo hafanyi), au huutafutia mahali katika maelezo ya chimbuko la mwanadamu. Uhuru haujaonyeshwa popote kama jambo kuu la jumla ya maisha ya Kikristo ambalo linapaswa kuonekana katika kila moja ya vitendo vyetu. Pengine hili ni jambo ambalo linachukuliwa kuwa la kawaida. Lakini suala la udhihirisho unaoonekana na dhahiri wa uhuru halichukuliwi kamwe kama sehemu ya kuanzia. . . . Ni mada ambayo imetoweka katika upeo wa Kikristo. Muumini hajali kujua kama yuko huru wala hatilii maanani hata kidogo kuhusu njia za kudhihirisha uhuru wake. Kwa maoni yangu hili ndilo jambo lenyewe linaloelezea uzembe wa maisha ya Kikristo, ukosefu wake wa maana, kushindwa kwake kuleta athari kubwa kwa jamii. Matendo ya upendo na huduma yanaweza kuzidishwa, haki inaweza kudhihirishwa, na imani inaweza kuonyeshwa, lakini hakuna hata moja ya haya yenye thamani yoyote bila uhuru.
~ Jacques Ellul. The Ethics of Freedom . Trans. by Geoffrey W. Bromiley. Grand Rapids: Eerdmans, 1976. uk. 104-105.
A. Ufafanuzi wa wito wa uhuru katika hadithi ya Kutoka, Kut. 3:2-10
1. Utambuzi wa utumwa wa kikatili chini ya mkono kandamizi wa Farao, Kut. 3:7 – Bwana akasema, “Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko
Made with FlippingBook Digital Publishing Software