Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Kipindi cha 4 : Wito wa Uhuru

47

Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao.”

2. Mungu anasikia kilio cha watu wake na hudhamiria kuwaokoa, Kut. 3:8-9 – nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa 3. Mungu anamtenga kiongozi wake maalum (Musa) ili kuwasilisha neno lake, kuonyesha ishara na ajabu zake ili kuwakomboa watu wake, Kut. 3:10 – Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri. 4. Mungu anawaweka huru watu wake ili wapate kumwabudu na kumwakilisha, Kut. 14:30-31 – Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa. 31 Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya Bwana juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha Bwana, wakamwamini Bwana, na Musa mtumishi wake.

B. Kanuni kwa watu wa Mungu leo

1. Uhuru kutoka Misri: Uhuru kutoka utumwani kupitia huduma ya Yesu Kristo, Lk. 4:18-19 – Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software