Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

48

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

a. Tumewekwa huru kutoka kwenye tabia za kimwili, udunia, na nguvu za dhambi (Rum. 6:1-13).

b. Tumewekwa huru kutoka katika kutawaliwa na adui (Yak. 4:8; 1 Pet. 5:8-9; 1 Yoh. 4:4).

c. Tumewekwa huru na hukumu ya hatia (Rum. 5:1; 8:1-4).

d. Tumewekwa huru kutoka kwenye ubatili na utupu wa dini (Flp. 3:2-7).

2. Uhuru ndani ya Kanaani: Kuishi katika uhuru wa Yesu Kristo, Gal. 5:1 – Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

a. Tuko huru kutembea na kuongozwa na Roho, Gal. 5.16-18 – Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana,

hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

b. Tuko huru kutii amri za Yesu (Yn. 13:34-35).

c. Tuko huru kumpenda Mungu na wengine kwa moyo wote na kwa njia zenye ubunifu, Gal. 5:13 14 – Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. 14 Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software