Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa
Kipindi cha 4 : Wito wa Uhuru
49
d. Tumewekwa huru ili kujinidhamisha kwa kusudi la utauwa, 1 Tim. 4:7-8 – Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. 8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
e. Tumewekwa huru ili kumjulisha Mungu kwa wengine, 1 Kor. 9:19 – Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
3. Kanuni za uhuru kwa waamini wote
a. Maisha ya Kikristo ni uzoefu wa badiliko na upya (1 Kor. 6:9-11).
b. Tuko huru katika Kristo, lakini si kila kitu kinajenga au kusaidia (1 Kor. 6:12; 10:23).
c. Tuko huru katika Kristo, lakini hakuna kitu chenye kuleta uraibu au chenye kutawala kinachopaswa kuwa na nguvu juu yetu (1 Kor. 6:12).
d. Tuko huru katika Kristo, lakini hatupaswi kujigamba ili kuumiza dhamiri za waumini walio na dhamiri dhaifu (1 Kor. 8:7-13).
e. Tuko huru katika Kristo, na tunapaswa kutumia uhuru wetu kuwapenda kaka na dada zetu katika Kristo (Gal. 5:13; 1 Kor. 10:24).
f. Tuko huru katika Kristo, lakini hatupaswi kuutumia kama kibali cha dhambi, bali kujiona sisi wenyewe kama watumwa wa Mungu (1 Pet. 2:16; Gal. 5:13).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software