Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

50

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

g. Tuko huru katika Kristo ili kumpa Mungu utukufu katika mambo yote (1 Kor. 10:31).

h. Tuko huru katika Kristo si ili kuwakosesha Wayunani au Wayahudi, bali kutumia uhuru wetu kwa ajili ya wokovu wao (1 Kor. 10:32-33).

C. Mifano halisi kuelezea wito wa uhuru

1. Mwenye pepo wa Wagerasi aliyeponywa, Mk. 5:15 17 – Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. 16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. 17 Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao. 2. Waamini wa Korintho, 1 Kor. 6:9-11 – Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. 11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu

3. Wito wa uhuru kwa viongozi, Mdo. 13:2 – Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.”

Made with FlippingBook Digital Publishing Software