Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

54

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

4. Tunapaswa kutangaza na kudhihirisha uhuru wa Agano Jipya katika Roho wa Mungu.

5. Uhuru wetu katika Kristo unapaswa kutuongoza kwenye kiwango kipya cha nidhamu binafsi na utauwa.

B. Kuhusianisha somo na maisha yako

1. Je, ninaelewa asili ya wito wa Mungu wa uhuru (kutoka kwenye sheria ya dhambi na mauti hadi maisha mapya na utakatifu katika Kristo)? Je, ninaelewa kwamba uhuru dhidi ya dhambi si ruhusa ya kufanya dhambi bali ni mwaliko wa kuishi kama mtumwa wa Kristo mwenyewe, anayeishi ili kumpendeza yeye na si kujipendeza mwenyewe? 2 Kor. 5:9 – Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.

2. Je, ni kwa namna gani ninaruhusu katika maisha yangu binafsi hali ya kujihesabia haki kwa kushika sheria, kuhukumu wengine, na matendo ya mwili kuingilia uhuru wangu katika Yesu Kristo?

3. Je, ninahisi hitaji la kutumia uhuru wangu katika Kristo kuwapata wengine, kuvuka vizuizi na mipaka ya utamaduni, matabaka, na rangi ili kuwashirikisha Habari Njema wale walio tofauti nami? Je, nina shauku ya kukumbatia kiwango kingine cha uhuru kwa ajili ya kuwahudumia wengine?

4. Je, nimewashirikisha marafiki na viongozi wangu upako huu na shauku ya kupenya tamaduni zingine kwa Injili ya Yesu Kristo?

5. Mungu ananiita kufanya nini hapa sasa hivi, kwa kuzingatia uhuru wangu katika Yesu Kristo?

Made with FlippingBook Digital Publishing Software