Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

Kipindi cha 6 : Wito wa Utumishi

79

B. Kuhusianisha somo na maisha yako

1. Je, nina sifa ya uaminifu, utumishi, na kuaminika katika familia yangu, kanisa, na jumuiya? Je, nimedhihirisha na hata sasa ninayo nia ya kuwatumikia wengine, nia ya kujitolea kwa niaba ya wale walio na mahitaji?

2. Je, ninatafsiri huduma katika misingi ya utoshelevu binafsi au katika misingi ya kujali mahitaji ya wengine?

3. Je, ninauhisi mzigo wa Bwana wa kutumia karama zangu kuchunga, kutunza, au kutoa uongozi katika Kanisa? Je, nimewashirikisha wengine kuhusiana na mzigo huu nilionao?

4. Je, ni katika maeneo gani hasa ninajihisi kutotoshea katika kutekeleza wito wa huduma maalum?

5. Je, viongozi wangu wamenipa taa ya kijani, njano, au nyekundu kuhusu suala la mimi kuelekea kwenye wajibu na huduma kubwa zaidi katika Kanisa?

6. Ikiwa nipo kwenye ndoa, je, mwenzi wangu anaonyesha kujali na kukubaliana nami kuhusu kuuendea wito wa huduma maalum katika Kanisa? Kwa nini ndiyo au sio?

7. Ninahitaji kupokea nini ili kuchukua hatua inayofuata kuelekea kutii wito wa Yesu juu ya maisha yangu kwa ajili ya huduma maalum? Je, nizungumze na nani sasa kuhusu kile ninachohisi kuhusu jukumu langu katika huduma na uongozi?

Made with FlippingBook Digital Publishing Software