Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kupitia Kanisa

78

Wito Halisi: Kumwakilisha Kristo na Ufalme Wake Kupitia Kanisa

1. Maisha ya kila mmoja wetu (na kwa hivyo fursa za huduma) ni ya kipekee: historia ya maisha yetu, mitandao ya mahusiano, uwezo binafsi, na fursa za huduma vinatofautiana.

2. Hakuna saizi hata moja inayotoshea vyote katika huduma; Mungu huwapa watu kazi maalum kwa makusudi yake na sababu zake.

3. Mungu anaweza kuwaita watu katika huduma kwa njia nyingi na kupitia namna nyingi.

4. Hatumdai Mungu chochote. Yeyote anayetumiwa na Mungu kwa njia yoyote anapaswa kushukuru kwa zawadi yake ya neema.

5. Bila kujali nafasi iliyotolewa, mamlaka yote yametolewa kwa madhumuni ya kuwafaidia na kuwajenga wengine (2 Kor. 13:10).

6. Kanuni ya utendaji kwa uongozi wote wa Kikristo ni utumishi, mtu kutoa maisha yake kwa manufaa ya ushirika (Mt. 20:26-28).

7. Roho Mtakatifu pekee ndiye huamua kina na upeo wa miito yetu binafsi kupitia mgao wa karama zake (2 Kor. 3:17; 1 Kor. 12:1-13).

8. Akiwa Bwana wa wote, Yesu Kristo ndiye anaongoza hatua za wanaume na wanawake watumishi wake, akiwawezesha kutimiza huduma zao apendavyo (Mt. 9:35-39).

9. Dhamira ya kweli na juhudi kamwe si kigezo cha huduma thabiti; bila maongozi ya Bwana na uwezesho wake, hatuwezi kuwa na huduma yenye matunda (2 Kor 3:4-5).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software